Wagombea 13 kati ya 15 waliojitokeza
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa Miguu wa
Wanawake Tanzania (TWFA) wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika juzi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati
ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, waliopitishwa kwenye nafasi ya uenyekiti ni
Isabellah Huseein Kapera, Joan Ndaambuyo Minja na Lina Paul Kessy.
Makamu Mwenyekiti ni Rose Kisiwa
wakati wanaowania nafasi ya Katibu Mkuu ni Amina Ali Karuma na Cecilia Oreste
Makafu. Mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Msaidizi, Macky Righton Mhango naye
amepita kwenye usaili huo. Aliyepitishwa kwenye nafasi ya Mhazini ni Rose
Stewart Msamila.
Furaha Francis na Zena Chande
wamepitishwa kuwania nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) wakati waliopita kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TWFA ni Triphonia Ludovick Temba, Rahim Salum Maguza na Sophia James Charles.
Hivi mchakato wa uchaguzi wa TWFA
uko katika kipindi cha kukata rufani ambapo ni kuanzia Oktoba 15-17 mwaka huu.
Rufani zinatakiwa zifike kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya
Oktoba 17 mwaka huu.
Wagombea wawili ambao hawakupitishwa
kwa ajili ya uchaguzi huo
unaotarajiwa kufanyika Novemba 4
mwaka huu ni Julliet Mndeme na Jasmin Soud walioomba ujumbe wa Mkutano Mkuu wa
TFF. Wagombea hao ambao pia walikuwa wamewekewa pingamizi hawakufika kwenye
usaili.